Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugiriki: UNHCR na wadau wajitahidi kuboresha maisha ya waomba hifadhi

Ugiriki: UNHCR na wadau wajitahidi kuboresha maisha ya waomba hifadhi

Wakati msimu wa baridi ukishika kasi , kuboresha maisha ya waomba hifadhi na wahamiaji kunaendelea kuwa kipeumbele cha kwanza kwa wadau wa masuala ya kibinadamu nchini Ugiriki na pia kusalia kuwa changamoto kubwa.

Watu wanaoishi kwenye mahema katika maeneo ya wazi wamehamishiwa kwenye makazi mbadala nay a mradi wa UNHCR, kwa ufadhili wa tume ya Muungano wa Ulaya shirika hilo limetoa makazi 20,000 yanayohitajika na wakimbizi na waomba hifadhi hao.

Hata hivyo UNHCR inasema changamoto bado zipo na wengi ya watu hao wanais hi kwenye makazi duni kama anavyofafanua William Spindler

(SAUTI YA SPINDLER)

“Hali inatofautiana kwa kiasi kikubwa, maeneo mengine yana hali duni sana na kukosa huduma kama ushauri nasaha, huduma za afya na ukalimani au hata kutokuwa na usalama unaostahili.”

Hadi sasa watu 2600 wamehamishiwa kwenye makazi mbadala na ifikapo mwisho wa mwaka idadi itaongezeka hadi 7500.