Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano ya Ninja yawafurusha watu 13,000 Congo:UNHCR

Mapigano ya Ninja yawafurusha watu 13,000 Congo:UNHCR

Mapigano yanayoendelea baina ya vikosi vya serikali ya Jamhuri ya Congo (ROC) na watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa zamani wanaojiita Ninjas yamewalazimisha maelfu ya watu kufungasha virago Kusini Mashariki mwa jimbo la Pool na kuathiri kilimo katika jimbo hilo lenye rutuba nchini humo.

Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema watu 13,000 waliotawanywa na mapigano hayo watakosa chakula muda si mrefu, na wakazi wa jimbo la Pool sasa wanakabiliwa na adha nyingine kama kukosa huduma za afya na elimu kwani walimu na wahudumu wa afya wamekimbia machafuko. William Spindler ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA SPINDLER)

“Katika wiki za karibuni maachafuko yameongezeka ikiwa ni pamoja na shambulio dhidi ya gari la jeshi lililosababisha vifo vya watu wawili, kwa sababu ya machafuko ya sasa mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesitisha shughuli zake wiki hii na hatutaweza kupeleka misaada hadi usalama utakapoimarika”