Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajira milioni 50 katika sekta ya afya zahitajika : ILO

Ajira milioni 50 katika sekta ya afya zahitajika : ILO

Utafiti uliofanywa wa shirika la kazi duniani ILO unaonyesha kuwa takribani ajira milioni 50 zenye kipato cha juu kwa mwaka wa 2016 zinahitajika huku huduma za afya zisizo na malipo zikitekelezwa na watu milioni 75 kote duniani.

Utafiti huo uliopewa jina Nguvu kazi ya afya, mwenendo wa kimataifa na kuhusisha nchi 185 inaonyesha kuwa hatua hiyo ni tishio katika kukabiliana na magonjwa yaambukizayo kwa kasi kama vile homa kali ya Ebola.

Xenia Scheil Adlung, ni mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo iliyowasilishwa kwa waandishi wa habari leo mjni Geneva, Uswis.

( SAUTI XENIA)

"Barani Afrika mathalani, afya makazini yaweza kukuza ajira milioni 16 na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Ajira nyingine milioni 27 zaweza kupatikana kufikia mwaka 2030.’’