Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu milioni 2.6 wametawanywa na machafuko bonde la Ziwa Chad

Zaidi ya watu milioni 2.6 wametawanywa na machafuko bonde la Ziwa Chad

Kwa mujibu wa tathimini ya kwanza ya kikanda ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, watu milioni 2,636,450 kwenye bonde la ziwa Chad wametawanywa na uasi wa kundi la Boko Haram , ndani ya eneo hilo lakini pia nje ya mipaka kama wakimbizi.

Tathimini hiyo inasema watu wengine zaidi ya milioni 1.2 wamerejea nyumbani baada ya kufungasha virago kutokana na machafuko, nah ii inafanya idadi ya watu wote walioathirika moja kwa moja na machafuko kufikia zaidi ya milioni 3.6.

Katika kuhakikisha inakidhi kikamilifu mahitaji ya watu wote waliotawanywa , IOM imefufua mkakati wake wa kufuatilia idadi ya watu wanaotawanywa na machafuko (DTM) ambao Nigeria ulianza Julai 2014, Chad Januari 2015 na Cameroon Novemba 2015.