UNHCR yapatia Uganda msaada wa magari

UNHCR yapatia Uganda msaada wa magari

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, nchini Uganda limepatia serikali ya Uganda magari yenye thamani ya dola milioni moja ili kurahisisha shughuli za ofisi ya Waziri Mkuu za kuhudumia wakimbizi. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Magari hayo yamekabidhiwa  kwenye sherehe iliyohudhuriwa na Kamishina wa Wakimbizi wa Uganda, David Kazungu na  Mwakilishi wa UNHCR Uganda Bornwell Kantande Jijini Kampala.

Kantande amesema Uganda yastahili kupata magari hayo sio tu kwa kusaidia wakimbizi bali pia jamii zinazowahifadhi kama njia ya kutambua ukarimu wao wa kuendelea kukiribisha wakimbizi.

Alisisitiza kwamba UNHCR, itaendelea na kanuni ya kutumia 30% ya rasilimali zao kuimarisha shule na huduma za afya na miundominu zingine kunufausha jamii zinazohifadhi wakimbizi.

Akigusia zaidi mzozo wa wakimbizi wa Sudan Kusini wanaomiminika kila uchao, Kamishna Kazungu amewataka wadau wote kutumia vyema magari yaliotolewa ili kuendeleza huduma kwa wakimbizi kati ya changamoto za rasilimali.