Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Daw Aung Aung San Suu Kyi sikiliza kilio cha wananchi Myanmar- UM

Daw Aung Aung San Suu Kyi sikiliza kilio cha wananchi Myanmar- UM

Umoja wa Mataifa umesema una wasiwasi mkubwa kuhusu hali inavyozidi kubadilika kwenye jimbo la kaskazini la Rakhine nchini Myanmar ambako vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu vinaripotiwa.

Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa umoja huo kuhusu Myanmar, Vijay Nambiar amesma hayo katika taarifa yake iliyotolewa jijini New York, Marekani hii leo.

Ametaka vikosi vya ulinzi kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kukubali maadili ya kimataifa huku vikiwa makini ili kuepusha ghasia pindi vinapohusika na raia.

Bwana Nambiar amesema ingawa uteuzi wa  jopo la uchunguzi la kitaifa umeibua maswali mengi kuhusu wajumbe na mamlaka yake, bado ana imani kuwa litatekeleza majukumu yake kwa uhuru ili kujenga imani miongoni mwa wakazi wa eneo hilo la Rakhine.

Mshauri huyo amesema anashawishika kuwa kiongozi mshauri wa Myanmar Aung San Suu Kyi anasikia na kuelewa hofu ya jamii ya kimataifa.

Hata hivyo amesema kitendo cha yeye kukataa mamlaka za Myanmar kuchukua hatua thabiti dhidi ya watu wenye misimamo mikali na kuridhia sheria za kujitetea kumeibua kukata tamaa kitaifa na kimataifa.