Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM Pakistan waomboleza abiria wa ndege ya PK-661

UM Pakistan waomboleza abiria wa ndege ya PK-661

Timu ya Umoja wa Mataifa nchini Pakistan imetuma salamu za rambirambi kwa wote waliopoteza ndugu, familia au marafiki kwenye ajali ya ndege ya shirika la ndege la kimataifa la Pakistan (PIA) ndege nambari PK-661 iliyokuwa ikisafiri kutoka Chitral kwenda Islamabad.

Wamesema Umoja wa Mataifa pia umepoteza wapendwa wake, miongoni mwao ni naibu kamishina wa Chitral, Osama Ahmed Warraich, ambaye alikuwa na jukumum muhimu kusaidia mashirika ya Umoja wa Mataifa ili yawasaidie watu wakati wa zahma za mafuriko na tetemeko la ardhi 2015.

Pia alisaidia katika kampeni ya chanjo ya kutokomeza polio pamoja na kuchagiza na kulinda utamaduni wa kipekee wa Chitral.

Awali akiwa msaidizi wa mkuu wa wilaya ya Peshawar, alisaidia sana kazi za Umoja wa Mataifa jimboni hapo.

Ujuzi wake, utu a urafiki wake utakumbukwa daima na kifo chake, cha mkewe na mtoto wake mdogo kimewauma wengi na kitaendelea kuhisiwa amesema Neil Buhne, mratibu mkazi na mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Pakistan.