Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yashiriki kampeni ya He for She kupinga ukatili dhidi ya wanawake

UNMISS yashiriki kampeni ya He for She kupinga ukatili dhidi ya wanawake

Wajumbe wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS wameshiriki Jumatano kampeni ya kimataifa dhidi ya ukatili dhidi ya wanawake ijulikanayo kama He For She kwa kutia saini fomu ya ahadi isemayo “Mi ni mmoja kati ya mabiloioni ya watu wanaoamini kwamba kila mtu amezaliwa huru na sawa na ntachukua hatua dhidi ya upendeleo wa kijinsia, ubaguzi na ukatili ili kuleta faida ya usawa kwa wote”.

Naibu kamanda wa vikosi vya UNMISS, Meja jenerali Chaoying Yang amewaambia walinda amani katika kikosi chake kwamba ni lazima wafanye kazi kwa juhudi zote kuhakikisha usawa huo wa kijinsia kwa wote unafikiwa...

(CHAOYING CUT 1)

“Usawa wa kijinsia ungekuwa umefikiwa kama wanawake hawakabiliwi na ukatili majumbani mwao, kufanya kazi za huduma sawa na wanawaume na kuwakilishwa ipasavyo katika ngazi za juu kwenye biashara na siasa”

Amewachagiza wote kuhakikisha mabadiliko yananzia kwao...

(CHAOYING CUT 2)

“Nawaomba wote tujizatiti kuchukua hatua dhidi ya ubaguzi wa kijinsia na ukatili ili tujenge dunia iliyo na haki zaidi na usawa”

Siku 16 za harakati ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake zitafikia kilele Disemba 10 mwezi huu.