Skip to main content

Baiskeli yakwamua wasichana dhidi ya madhila Tanzania

Baiskeli yakwamua wasichana dhidi ya madhila Tanzania

Nchini Tanzania mshindi wa tuzo ya kimataifa UNICEF inayotambua juhudi za kuokomeza ndoa za utotoni Rebeca Gyumi amesema mradi walioanzisha wa msichana mmoja baiskeli moja umeanza kupunguza madhila wanayopata wanafunzi wa kike.

Akihojiwa na idhaa hii, Bi. Gyumi ambaye anaongoza shirika la Msichana Initiative amesema wameanzia mkoani Dodoma katika shule ya Mwitikira wakilenga zaidi madarasa ya awali ya shule za sekondari na wanafunzi wenye chagamoto nyingi..

(Rebecca-1)

Amesema licha ya mafanikio bado kuna changamoto ikiwemo uelewa wa jamii akisema msaada wao hujumuisha pia pampu za baiskeli lakini..

(Rebecca-2)

Rebecca amesema hizo ni changamoto ndani ya mafanikio lakini hawakati tamaa hivyo wana mpango wa kupanua wigo wa msaada huo.