Mauti yakinifika nirejesheni kwetu- Fatima
Mapigano ya kila uchao huko Mosul, nchini Iraq yamekuwa mwiba si kwa vijana pekee bali pia watu wazima. Wakazi wa Mosul wamesaka hifadhi kwingineko kwani makwao milio ya makombora na mashambulizi yasiyokoma yamesababisha ugenini kuwa nyumbani, japo kwa muda usiofahamika. Miongoni mwa wakimbizi hao ni Fatima Mehemed ambaye sasa yuko kambi ya Qay Mawa inayohifadhi wakimbizi zaidi ya 4,600 na ndoto yake ni kwamba mauti yakimkuta arejeshwe nyumbani. Je hali ilikoje kambini ambako Umoja wa Mataifa unajitahidi kukidhi mahitaji? Assumpta Massoi na simulizi kwenye makala hii.