Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Korea: Familia zinahisi machungu ya kutengana kila uchao

Korea: Familia zinahisi machungu ya kutengana kila uchao

Umoja wa Mataifa umeonya kwamba familia zilizosambaratishwa na miongo ya kutenganishwa kwa lazima kwenye rasi ya Korea huenda wasiungane tena na familia zao kufuatia mvutano unaoongezeka kwenye eneo hilo.

Tangu vita vya Korea baina ya Kaskazini na Kusini mwaka 1953 vilivyoigawa mapaqnde mawili nchi hiyo karibu familia 130,000 zimeorodhjeshwa kwa ajili ya kuunganishwa tena na familia zao.

Zaidi ya nusu wamefariki dunia bila kutimiza lengo hilo imesema ripoti ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa. Imeongeza kuwa kila siku inayopita machungu kwa familia zilizotenganishwa na jamaa zao miaka 60 iliyopita ni kama msumari wa moto juu ya kidonda.

Akizungumzia ripoti hiyo Kamishina mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein, ameonya kwamba kikwazo kikubwa katika kuziunganisha tena familia hizo ni ongezeko la mivutano ya kisiasa na kijeshi kwenye rasi ya Korea ambayo imezuia majadiliano baina ya nchi hizo mbili.

Tangu mwaka 2000 ni familia 100 tuu ndizo zilizoweza kuonna na jamaa zao katika kila upande wa mpaka na Zaidi ya nusu ya watu wa familia hizo hyivi sasa wana umri wa Zaidi ya miaka 80.