Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuboresha afya na hatua muafaka kipindupindu kitakwisha Haiti: Nabarro

Kuboresha afya na hatua muafaka kipindupindu kitakwisha Haiti: Nabarro

Kukiwepo rasilimali za kuwezesha hatua muafaka na kuboresha masuala ya maji na usafi kwa wahaiti wote basi kipindupindu kitaondoka nchini nchini humo.

Kauli hiyo ni kwa mujibu wa David Nabarro, mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na mipango ya kukabiliana na kipindupindu Haiti.

Bwana Nabaro ametoa kauli hiyo baada ya Umoja wa Mataifa kuomba radhi wiki iliyopita kwa kutowajibika ipasavyo tangu mlipuko wa maradhi hayo Haiti miaka sita iliyopita na hadi sasa watu zaidi ya 9000 wamepoteza maisha kutokana na kipindupindu.

Bwana Nabarro anaeleza endapo kuongeza timu inayosaidiwa na Umoja wa Mataifa kupambana na ugonjwa huo Haiti kumeleta mabadiliko yoyote..

(SAUTI YA NABARO)

“Idadi kubwa ya watu walioripoti kuwa wanaugua, sasa wanaweza kupata tiba ndani ya saa 48 tangu ugonjwa wao uripotiwe. Licha ya kimbunga, tumeshuhudia idadi ya visa ikipungua.”

Umoja wa Mataifa umeahidi kutoa msaada wa msaada wa haraka kwa sasa lakini pia wa muda mrefu kwa waathirika wa ugonjwa huo.