Skip to main content

Ban akaribisha majadiliano ya upatanishi DRC

Ban akaribisha majadiliano ya upatanishi DRC

Ikiwa ni majuma mawili kabla ya mwisho wa mhula wa pili wa Rais wa Jmahuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC Joseph Kabila, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha muendelezo wa upatanishi unaoratibiwa na kanisa katoliki nchini DRC , CENCO ili kufanikisha makubaliano jumuishi kwa ajili ya uchaguzi nchini humo. Amina Hassan na taarifa kamili.

( TAARIFAYA AMINA)

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu, Ban amesema anatambua kuwa Rais wa DRC Joseph Kabila ameeleza usaidizi na kuhamasisha upatanishi wa CENCO pamoja na utayari wa upinzani kusalia katika majadiliano.

Katibu Mkuu ameeleza kadhalika kuwa yu tayari kutoa usaidizi kwa CENCO na kuwataka wadau wa kisiasa  nchini  DRC kuhusika katika mchakato huo.