Zambia iongeze mapato ili ijikwamue kiuchumi- Ripoti

7 Disemba 2016

Benki ya dunia imesema Zambia inahitaji kuongeza kiwango cha ukusanyaji mapato ya ndani  ili iweze kukidhi viwango vya sasa vya matumizi ya serikali.

Ripoti ya benki hiyo kuhusu kuongeza ukusanyaji mapato Zambia kwa lengo la kukwamua uchumi, imesema ukuaji uchumi nchini humo kwa mwaka huu wa 2016 umeendelea kusuasua, sababu ikiwa ni mazingira makali ya uchumi duniani sambamba na changamoto za ndani kama vile katizo la umeme.

Hata hivyo mchumi mwandamizi wa benki ya dunia Gregory Smith amesema ingawa mwelekeo wa bajeti ya 2017 kwenye ukusanyaji mapato ya ndani unatia matumaini, bado serikali ichukue hatua zaidi kwa kuiamarisha elimu ya mlipa kodi ili watu wafahamu umuhimu wa kodi na walipe, halikadhalika kuweka mfumo bora wa kodi na kuboresha uwazi kwenye ufuatiliaji katika setka ya madini.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter