Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upungufu wa madini wachochea usonji

Upungufu wa madini wachochea usonji

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano kuhusu usonji barani Afrika ambapo mmoja wa watoa mada amezungumzia umuhimu wa madini katika kukabiliana na ugonjwa huo.

Akizungumza na Idhaa hii baada ya mkutano huo, Dkt. Joel Wallach kutoka taasisi ya kimataifa ya ufumbuzi wa afya amesema ukosefu wa madini ya Potasia, Fosforasi na Nitrojeni kwenye ubongo ni chanzo akisema..

(Dkt. Wallach -1)

"Watu waliokuwa na afya zaidi walikuwa ni watu wa asili, wakitumia kuni kama nishati, na kutumia majivu kama kama mbolea, na kile ambacho watu hawakufahamu nap engine hadi sasa ni kwamba mimea ilifyonza madini hayo na watu walipokula vyakula vyake walipata virutubisho, sasa tuna umeme, hakuna tena majivu ya kuni na ndipo usonji ukaanza kuwa tatizo kubwa ulimwenguni."

Hivyo amesema suluhisho la ugonjwa huo barani Afrika ni kwa mama kupata madini na changamoto zake na ndiyo maana wanapitia Umoja wa Mataifa ili kupitia mradi huo...

(Dkt. Wallach 2)

"Mama apate madini haya kabla ya hajabeba ujauzito, ili kusiwe na mtoto mwenye usonji. Changamoto ni sera za serikali ambazo zitazuia vidonge ya madini haya kuingia ama kuweka mahitaji ya juu ambayo yatahitaji matumizi ya mamilioni ya dola kupata kibali cha kuingiza bidhaa hizi"