Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSMIL irejee Libya ili kuongeza ufanisi: Kobler

UNSMIL irejee Libya ili kuongeza ufanisi: Kobler

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Martin Kobler amesema licha ya kuwepo kwa matumaini ya amani na usalama nchini Libya bado kuna shaka na shuku.

Akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililokutana leo kuangalia mustakhbali wa Libya, Bwana Kobler amesema mkataba wa kisiasa wa Libya bado unasalia muundo pekee wa kupata suluhu ya kudumu nchini humo.

Amesema hata wakosoaj i wakuu wa mkataba huo wanasalia kuamini kuwa ndio suluhu pekee hivyo ametoa mapendekezo sita ya kufanikisha amani na usalama Libya.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kuhakikisha hoja za kisiasa ambazo hazijapatiwa jawabu zishughulikiwe, suala la vikundi vilivyojihami Tripoli linasuluhishwa kwa kuuanzisha walinzi wa Rais.

Halikadhalika ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL ambao yeye ni kiongozi wake..

(Sauti ya Kobler)

“Nataka kusisitiza umuhimu wa UNSMIL kurejesha makao yake huko Tripoli kwa awamu pindi hali ya usalama itakapokuwa shwari. Tunaweza kuwa na tija zaidi tukiwa Tripoli kuliko tulivyo Tunis. UNSMIL lazima irejee Libya na tufanye sasa kwa kusaidia wadau wetu katika mazingira haya magumu. Utulivu unaweza kufanikiwa zaidi kwa jamii ya kimataifa ikiwemo nchini humo na si ughaibuni.”