Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fedha zahitajika haraka kunusuru mgao wa chakula kwa wakimbizi Kenya:WFP

Fedha zahitajika haraka kunusuru mgao wa chakula kwa wakimbizi Kenya:WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limelazimika kupunguza tena mgao wa chakula kwa wakimbizi nchini Kenya kutokana na upungufu wa ufadhili . Rosemary Musumba na taarifa kamili

(TAARIFA YA ROSE)

WFP kuanzia mwezi huu imepunguza kwa nusu mgao wa chakula kwa wakimbizi 434,000 kwenye kambi za Dadaab na Kakuma nchini Kenya na chakula walichonacho kitatosheleza hadi Februari.

Kwa mujibu wa Annalisa Conte mwakilishi na mkurugenzi wa WFP Kenya dola milioni 13.7 zinahitajika haraka ili kukidhi mahitaji ya chakula na fedha taslimu kwa wakimbizi hao kati ya mwezi huu wa Desemba na April.

Ametoa wito kwa wahisani kusaidia wawezavyo ili kuwanususu maelfu ya wakimbizi wanaotegemea msaada wa WFP ili kuishi..