Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yamfungulia mashtaka raia wa Uganda ikimtuhumu kuhusika na vita

ICC yamfungulia mashtaka raia wa Uganda ikimtuhumu kuhusika na vita

Mahakama ya kimataifa ya  uhalifu ICC  imemfungulia kesi raia wa Uganda  Dominic Ongwen mwenye umri wa miaka 70 ikimtuhumu kuhusika na uhalifu wa kivita kaskazini mwa Uganda kati ya mwaka 2000 na 2005 wakati akiwa kamanda wa waasi wa Lord’s Resistanace Army LRA.  Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

 Kwa mujibu wa taarifa ya ICC , jopo la majaji limeridhika kwamba mtuhumiwa anaelewa asili ya makosa anayotuhumiwa ikiwemo ubakaji na utumikishaji watoto vitani ambayo ameyekana.

Awali Jaji anayeongoza kesi hiyo Bertram Schmitt, amefafanua kuwa madai ya upande wa utetezi kuwa mtuhumiwa haelewi mashtaka hayana ukweli kwani.

(SAUTI JAJI SCHMITT)

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 16 mwakani, ambapo upande wa mashtaka utaanza kwa kuwasilisha ushahidi wake na kutoa wito kwa mashahidi wajitokeze.

Mwenendo wa kesi hiyo ulitangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari katika maeneo sita tofauti kaskazini mwa Uganda na mawili jijini Kampala.