Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kauli za wanasiasa dhidi ya wahamiaji Australia zatia hofu: Ruteere

Kauli za wanasiasa dhidi ya wahamiaji Australia zatia hofu: Ruteere

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu mifumo ya kisasa ya ubaguzi, ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na hali zingine za kutovumiliana Bwana Mutuma Ruteere amesema anatiwa hofu na kauli za baadhi ya viongozi wa kisiasa nchini Australia dhidi ya wahamiaji.

Akizungumza Jumanne na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa mjini Canberra Australia mwishoni mwa ziara yake ya kufanya tathimini ya hali ya masuala ya ubaguzi nchini humo amesema kauli za wanasiasa hao zinawalenga wahamiaji wapya wanaowasili na hasa Waislam. Amesema ni muhimu hali hiyo ikakoma mara moja

(RUTEERE CUT-1)

Na kisha akatoa wito kwa serikali ya Australia na vyama vyote vya kisiasa

(RUTEERE CUT-2)