Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Filamu ya Beckham yachagiza kukomesha ukatili dhidi ya watoto

Filamu ya Beckham yachagiza kukomesha ukatili dhidi ya watoto

Filamu mpya ye ujumbe mzito ikimshirikisha balozi mwemwa wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF David Beckham imetolewa leo ili kuelezea hali halisi kwamba unyanyasaji wa kimwili na kisaikolojia unaweza kuacha kovu la milele kwa watoto.

Katika sekunde 60 za filamu hiyo ya UNICEF, maonyesho ya vitendo vya kikatili dhidi ya watoto vinaonekana kama michoro juu ya mwili David Beckham, wakati michoro ya Beckham mwenyewe ni alama iliyochaguliwa kuwakilisha furaha au kumbukumbu muhimu. Mamilioni ya watoto wanabeba michoro au alama ambazo hawakuzichagua: makovu ya muda mrefu ya ukatili na unyanyasaji.

mifano kwa michoro katika filamu depict zote aina ya kawaida sana ya vurugu ambayo wavulana na wasichana kuvumilia katika maeneo ambapo wanapaswa kuwa salama - nyumba zao, shule, online na katika jamii zao.

Vikaragosi katika filamu hiyo vinaonyesha hali halisi ya ukatili ambao wavulana na wasichana wanaupitia katika maeneo ambayo wanapaswa kuwa salama, kama majumbani kwao, shuleni, kwenye mitandao na kwenye jamii zao.

David Beckham na UNICEF wanawataka watu kuisambaza filamu hiyo kwenye mitandao ya kijamii ili kufikisha ujumbe.