Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu lapata rais na makamu mpya kwa 2017

Baraza la haki za binadamu lapata rais na makamu mpya kwa 2017

barazahakiBaraza la haki za binadamu leo Jumatatu limechagua uongozi mpya kwa mwaka 2017. Balozi Joaquín Alexander Maza Martelli, mwakilishi wa kudumu wa El Salvador kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa Geneva ndiye atakayekuwa Rais wa baraza hilo kuanzia Januari Mosi 2017.

Baaraza hilo pia limemteua balozi Moayed Saleh wa Iraq, Balozi Amr Ahmed Ramadan wa Misri, Balozi Shalva Tsiskarashvili wa Georgia, na Balozi Valentin Zellweger wa Uswis kushikilia nafasi ya makamu wa Rais wa chombo hicho cha haki za binadamu.

Mabalozi wote watano watahudumu kama wajumbe wa taaisi ya baraza la haki za binadamu kuanzia Januari mosi hadi Desemba 31 mwaka 2017 wakati wa mzunguko wa 11 wa baraza hilo.

Akizungumza wakati wauteuzi huo ya balozi Choi Kyonglim (Jamhuri ya Korea), ambaye amekuwa Rais wa baraza kwa mwaka 2016 amekumbushia jinsi baraza hilo linavyoendelea kukabiliana na ongezeko la changamoto za haki za binadamu na utu kote duniani , kukichochewa na migogoro inayoendelea na vita vipya vinayoibuka, mashambulizi ya kigaidi, mtafaruku wa wakimbizi, matatizo ya kkiuchumi na ukandamizaji wa kisiasa.