Ahadi ya kuimarisha usalama wa nyuklia yatolewa :IAEA

5 Disemba 2016

Mawaziri kutoka serikali mbalimbali duniani wameahidi kuimarisha zaidi usalama wa nyuklia kimataifa, ikiwa ni pamoja na kukabiliana na usafirishaji haramu wa nyuklia na vifaa vingine vinavyoweza

kutengeneza nyuklia. Ahadi hiyo imetolewa Jumatatu na kupitishwa azimio maalumu la mawaziri kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu usalama wa nyuklia :ahadi na hatua kwenye shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA.

Mkutano huo unaoendelea hadi Ijumaa mjini Vienna, Austria umewaleta pamoja washiriki 2000 kutoka mataifa zaidi ya 130 nchi wanachama na mashirika 17 ya kimataifa, kikanda na asasi za kiraia.

Washiriki hao wanatathimini hali ya usalama wa nyuklia kimataifa na kubadilishana mawazo kuhusu mikakati na masuala ya kuyapa kipaumbele ili kuimarisha usalama.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter