Skip to main content

Jamii ya asilia ni walinzi wa misitu: Martha

Jamii ya asilia ni walinzi wa misitu: Martha

Mkutano wa nchi wanachama wa mkataba wa bayoanuai unaendelea nchini Mexico ambapo wadau mbalimbali wanakutana kujadili namna ya kuboresha sekta hiyo kabla ya mkutano wa nchi wanachama COP 13 mjini Cancun nchini humo mwezi huu.

Miongoni mwa washiriki katika mkuatno huo ni Martha Ntoipo, mwakilishi wa jamii ya wafugaji nchini Tanzania kutoka taasisi ya wafugaji na maendeleo (PIDO) ambaye pia anawakilisha jamii za watu wa asili.

Bi Ntoipo anataja kile ambacho jamaii ya watu wa asili inakitarajia baada ya mkutano.

( SAUTI MARTHA)