Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola bilioni 22.2 zahitajika 2017 kwa masuala ya kibinadamu: OCHA

Dola bilioni 22.2 zahitajika 2017 kwa masuala ya kibinadamu: OCHA

Ombi la kimataifa la mkakati wa kushughulikia masuala ya kibinadamu kwa mwaka 2017 limezinduliwa leo mjini Geneva Uswisi na mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa OCHA Stephen O'Brien.

Ombi hilo ambalo ni kubwa zaidi kuwahi kutolewa , lililozinduliwa wakati wa kutoa taarifa ya mtazamo wa kimataifa masuala ya kibinadamu linahitaji dola bilioni 22.2, ili kushughulikia mahitaji katika nchi 33.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo O’Brien amesema

(SAUTI YA O’BRIEN)

“Tunakabiliwa na wakati wa madhila makubwa na machungu kimataifa, licha ya mafanikio katika sehemu zingine watu wengi zaidi wamekwama katika mzunguko wa kutojiweza na kuhitaji msaada. Mbali ya vita pia tunaghubikwa na hofu ya majanga ya asili”

Miongi mwa nchi zitakazofaidika ni za Afrika Kusini mwa jangwa la sahara ambako kuna mipango madhubuti afisa wa masuala ya kibinadamu wa OCHA ni Lily Adhiambo

(SAUTI YA LILY ADHIAMBO)

Zaidi ya watu milioni 128 wanahitaji msaada kote duniani.