Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutunza udongo iwe utamaduni wetu: Ban

Kutunza udongo iwe utamaduni wetu: Ban

Usimamizi wa udongo endelevu utasongesha agenda ya 2030 ya maendeleo endelevu na mkataba wa mabadiliko ya tabianchiwa Paris amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku ya udongo duniani leo Jumatatu Desemba tano. Taarifa zaidi na Selina Cheroboni

( TAARIFA YA SELINA)

Ban amesema ni muhimu utunzaji wa udongo uwe utamaduni wa dunia ili kuongeza matumizi ya rasilimali hiyo, kuitunza na kuilinda kwa muda mrefu.

Katibu Mkuu amesisitiza kuwa katika dunia ya sasa ambayo idadi ya watu inaongezeka, hali ya hewa inabadilika na chakula zaidi kinahitjaika kwahiyo udogo wenye rutuba  ni muhimu ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma inayotolewa na udongo.

Ameshauri kuwa katika kuulinda udongo mimea ya jamii yakunde itumike kwani yaweza kuongeza rutuba huku pia ikiwezesha afya na milo yenye virutubisho.