Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apongeza Gambia kwa uchaguzi wa amani.

Ban apongeza Gambia kwa uchaguzi wa amani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Bna Ki-moon amewapongeza watu wa Gambia kwa kufanya uchaguzi mnamo Disemba mosi kwa amani na kufuata sheria.

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imemnukuu akipongeza tume huru ya uchaguzi kwa kuhakikisha kila kitu muhimu kimeandaliwa na kuratibu vyema uchaguzi wenye mafanikio.

Ban pia amempongeza Rais mteule Adama Barrow kwa kuchaguliwa kwake pamoja na kumpongeza Rais Yahya Jammeh kwa ujumbe wake wa kumpongeza Bwana Barrow.

Amesisitiza utayari wa Umoja wa Mataifa kuendelea kusaidia watu na serikali ya Gambia katika juhudi zao za kukuza haki za binadamu, kufanikisha maendeleo endelevu, kuimarisha utawala bora na utawala wa sheria nchini humo.