Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Ukimwi duniani

Siku ya Ukimwi duniani

Tumbuizo za hamasa zilitamalaki katika moja ya matukio makao makuu ya Umoja wa Mataifa, ambapo wadau walikusanyika kujadili mbinu za kukabiliana na Ukimwi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani yanayofanyika Disemba Mosi kila mwaka.

Umoja wa Mataifa unasema jumla ya watu milioni 78 kote duniani wanaishi na virusi vya ukimwi ( VVU) huku wengine milioni 35 wakiwa wamefariki dunia tango gonjwa hilo ligundulike miaka 35 iliyopita.

Katika ujumbe wake wa maadhmisho ya siku ya ukimwi duniani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kutokomeza Ukimwi ni moja ya malengo ya maendeleo endelevu  SDGs, linalotaka watu milioni 30 kupatiwa tiba ifikapo mwaka 2030.

Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya Ukimwi, UNAIDS linasema changamoto sasa ni kufikia vijana barubaru… hususan nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ambako ndio makala yetu inaanzia wiki hii kwa kujikita Uganda… John Kibego

anaangazia kiwango cha maambukizi na hatua zainazochukiliwa na taifa hilo.

(PACKAGE KIBEGO)

Nchini Tanzania tunajiunga na Nicolas Ngaiza wa redio washirika Kasibante Fm ya mkoani Kagera ambaye  anaangazia maambukizo hususan miongoni mwa vijana barubaru, akianza kwa kuhoji uwepo wa mbinu iliyopendekezwa hivi karibuni ya mgonjwa kujipima mwenye VVU.

( PACKAGE NGAIZA)