B Flow atumia kipaji chake kupinga ukatili wa kijinsia

2 Disemba 2016

Ukatili wa kijinsia ni moja ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu ambapo dhirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA limesema ni wakati wa kubadili hali hiyo iliyoota mizizi sehemu nyingi ulimwenguni..

Kwa mantiki hiyo wakati dunia ikizingatia siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana kuanzia Novemba 25 hadi Disemba 10 UNFPA imewaenzi wanaharakati 16 ambao wanachagiza mabadiliko. Mmoja wa wanaopaza sauti ni mwanamuziki B Flow kutoka Zambia ambaye anapaza sauti ya wasio na sauti kupitia nyimbo. Basi ungana na Rosemary Musumba katika makala hii.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter