Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNODC na WFF waafikiana kupima kiwango cha usafirishaji haramu wa watu

UNODC na WFF waafikiana kupima kiwango cha usafirishaji haramu wa watu

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kukomesha utumwa hii leo na kushughulikia uhalifu huo mamboleo ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC na wakfu wa Walk Free Foundation (WFF) wametangaza kutia saini muafaka ambao utawezesha mashirika hayo kufanya kazi pamoja kukadiria idadi ya waathirika wa usafirishaji haramu wa watu.

Kwa kuzingatia kazi zinazofanywa na mashirika yote mawili, kuanzisha njia mpya ya kupima uhalifu huu wa siri, mkataba unahusisha kutumia njia za kawaida, mbinu za ubunifu na timu ya kuweka makadirio ya biashara ya binadamu kwa kuanzia katika nchi nne za Ulaya.

Hii itatoa takwimu zinazohitajika kuhusu biashara haramu ya binadamu katika ngazi ya kitaifa na pia kujtoa ufahamu wa jinsi ya kupima uhalifu huu mkubwa. Mambo yote haya ni muhimu kwa mafanikio ya malengo ya maendeleo endelevu.

Mbinu hiyo mpya itakayoptumika inajulikana kama “Mifumo mbalimbali ya makadirio” ambayo mara nyingi hutumika kupima idadi ya watu isiyojulikana. Makadirio yayaliyowahi kufanyika yanaonyesha kwamba kuna waathirika wa usafirishaji haramu wa binadamu kati ya 10,000 na 13,000 nchini Uingereza na zaidi ya 17,000 nchini Uholanzi.