Skip to main content

Ukatili wa kingono Sudan kusini umefurutu ada-UM

Ukatili wa kingono Sudan kusini umefurutu ada-UM

Ukatili wa kingono umefurutu ada Sudan Kusini na dunia inahitaji kuchukua hatua haraka imesema tume huru ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini humo, baada ya kukutana na wanawake manusura wa ukatili huo nchi nzima.

Kiwango cha ubakaji dhidi ya wanawake raia na aina yenyewe ya ubakaji unaofanywa na magenge ya watu wenye silaha kutoka katika makundi yote kinachukiza na kutisha na kibaya zaidi hakuna anayekasirishwa na ukatili huo, amesema mwenyekiti wa tume hiyo Yasmin Sooka.

Akizungumza na kujibu maswali ya waandishi wa habari mjini Nairobi Kenya Bi Sooka amesema mwezi Juali walipobakwa wafanyakazi wa misaada wa kimataifa mjini Juba kulikuwa na kun’gaka na kulaaniwa kwa kitendo hicho , lakini ukweli wa mambo ni kwamba wanawake wa Sudan Kusini wanakabiliwa na ukatili huo kila siku na dunia inafumba machonao hawana pakukimbilia

(SAUTI YA YASMIN )

“Hali halisi ni kwamba hadhi ya wanawake haiku juu , jinsi wanawake wanavyoolewa mapema katika umri mdogo kwa ajili ya ng’ombe, mbuzi , katika kesi nyingi za ubakaji kwa sababu wanawake wanajua hawawezi kwenye kwenye mamlaka, kuna machifu wa kimila wa makabila mbalimbali wanaotatua kesi hizo na kwa bahati mbaya katika ubakaji wakati mwingine inaamuliwa kulipa tu gharama za mahakama au kitu kidogo kama dola 50 au 60 na kinachofanyika ni kupunguza uzito wa ukweli kwamba huo ni uhalifu mkubwa”

Sasa tume hiyo inataka kutoa wito wa kuundwe timu maalumu ya uchunguzi kwenda Sudan Kusini kukusanya ushahidi wa ubakaji ili kupata msingi wa kuwafikisha mbele ya sheria wahusika siku za usoni.