Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi unatoa fursa ya kufikia malengo ya SDG: ESCAP

Uchumi unatoa fursa ya kufikia malengo ya SDG: ESCAP

Hali imara ya kiuchumi katika kipindi cha pili ya mwaka wa 2016 inatoa fursa ya kuelewa hali ya kiuchumi, kijamii, kimazingira na vipimo vya utawala ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu ipasavyo. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya mwisho wa mwaka huu iliyo kwenye chapisho lao la utafiti la tume ya uchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa  kwa ukanda wa Asia-Pasifiki (ESCAP).

Ripoti hiyo inasema sera za kodi za maendeleo, utawala bora na ufanisi wa kiuchumi vinaweza kusaidia uchumi kufanya maendeleo katika kushirikisha na kuelekea kwa maendeleo endelevu.

Ripoti hiyo imeongezea kuwa mahitaji ya ndani na msaada wa sera vimesababisha uchumi wa mataifa yanayoendelea kukua kwa kasi ya kutosha chini ya asilimia 5 licha ya uchumi wa dunia na ukuaji wa biashara dhaifu. Ukuaji wa uchumi wa kanda hiyo ukiongozwa na China na India, umekuwa tulivu na kusababisha mtazamo chanya  kwa nchi za Asia na Pasifiki mwaka kwa 2017.

Akiongoza uzinduzi huo huko mjini Bangkok, Daktari Shamshad Akhtar, katibu mkuu na mtendaji wa ESCAP amesisitiza kuwa licha mtazamo chanya, athari za baadhi ya hatari haipaswi kupuuzwa, hali tete ya fedha inaweza kuibuka upya kutokana na kutokuwa na uhakika wa sera za nje zikiwemo zile zinazohusiana na 'Brexit' mazungumzo barani Ulaya na utawala mpya Marekani.