Skip to main content

Yoga yajumuishwa katika turathi za tamaduni

Yoga yajumuishwa katika turathi za tamaduni

Yoga imejumuishwa katika orodha ya Umoja wa Mataifa inayolinda tamaduni na mila kutoka sehemu mbalimbali duniani. Utamaduni huo wa kale ambao huusisha mwili, akili na hisia ulioanzia India ni miongoni mwa mambo matano yaliyoandikwa kujumuishwa Alhamisi kwenye orodha ya turathi za tamaduni zisizogusika.

Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa kamati inayofuatilia orodha hiyo ambayo inakutana mjini Addis Ababa, Ethiopia wiki hii. Yoga inaleta kutafakari, udhibiti wa pumzi, kuimba na mbinu nyingine ambayo kamati imesema ni "msingi unaounganisha akili, mwili na roho kwa ajili ya afya ya kiakili, kiroho na kimwili’

Kiasili yoga hufunzwa kutoka kwa mwalimu au mtaalamu kwenda kwa mwanafunzi , lakini leo hii watu wanajifunza na kuifahamu yoga kupitia mahekalu maalumu, vituo vya kijamii na maeneo mengine. Mambo mengine yaliyojumuishwa katika orodha hiyo ni utamaduni wa kulisha ndege uliotawala kwenye nchi kama Emarati, Ufaransa, Ureno na Syria, lakini pia mieleka ya kitamaduni kutoka Kazakhstan ijulikanayo kama kuresi.