Mpango mpya wa WFP wasaidia walio na njaa Nigeria

Mpango mpya wa WFP wasaidia walio na njaa Nigeria

Watu zaidi ya 45,000 wamepokea msaada wa chakula au lishe ya kuokoa maisha Kaskazini mwa Nigeria wiki iliyopita , kupitia mkakati mpya wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP wa kuwafikia walio vijijini na maeneo ambayo ni vigumu kuyafikia kutokana na zahma ya kundi la boko Haram.

Kwa msaada wa shirika la kuhudumia watoto UNICEF, WFP imeandaa mkakati wa haraka wa kupeleka msaada wa chakula , lishe na huduma ya afya kwa watu wanaohitaji zaidi kwenye majimbo ya Borno na Yobe , kwa kusafirisha kwa ndege timu ya wataalamu kwenye maeneo ya vijijini zaidi ambao wamekuwa huko kwa siku sita na msaada umefikishwa kwa njia ya barabara.

Mkakati huo mpya unalenga maeneo ambayo msaada haujawahi kufika au kufikika ni vigumu.

Kwa mujibu wa WFOP mkakati huo unasaidia kuepusha baa la njaa na unalenga kuwafikia maelfu ya watu wanaokabiliwa na njaa ambao wamekwama katika maeneo hayo kutokana na kutokuwepo usalama na hawajakuwa na msaada wowote kwa miezi kadhaa sasa.

Watu takribani milioni moja hadi milioni 1.8 wanahitaji msaada wa haraka wa chakula kwenye jimbo la Borno na Yobe