Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udhibiti holela wa wahamiaji ni muhimu katika vita dhidi ya ukimwi:IOM

Udhibiti holela wa wahamiaji ni muhimu katika vita dhidi ya ukimwi:IOM

Udhibiti hafifu wa suala la uhamiaji unaweza kuchangia athari za ukimwi kimataifa, lakini uhamiaji wenyewe sio sababu ya ugonjwa huo amesema mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM William Lacy Swing , katika siku ya ukimwi duniani Desemba Mosi.

Amesema ni muhimu kusisitiza kwamba kitendo cha uhamiaji hakisababishi ukimwi, hata hivyo hali ya kijamii na kiuchumi, kisiasa na kimazingira inauhusiano na kuhama kwa watu na kunaweza kuathiri afya na kuwaweka hatarini kupata maradhi ya ukimwi.

Ameongeza kua IOM tayari inafanya kila njia kudhibiti hali hiyo lakini bado kibarua kipo, kwani wahamiaji wanapokimbia makwao iwe kutokana na vita, majanga au hali ya kiuchumi wanapoteza kila uhusiano na familia zao na wanalazimika kuishi katika mazingira, mila, sheria na utamaduni tofauti.

Na katika jamii zinazowahifadhi mara nyingi hutengwa na kubaguliwa na hujikuta katika mazingira magumu kifedha, kiucsalama na wakiishi kwa hofu ya kukamatwa au kurejeshwa nyumbani kwa nguvu.