Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kauli kuhusu DRC zinalenga kuona amani inadumu- MONUSCO

Kauli kuhusu DRC zinalenga kuona amani inadumu- MONUSCO

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO umesema shaka na shuku juu ya kile kinachoendelea nchini humo kinasababisha kauli mbali mbali kutoka jamii ya kimataifa, lakini zenye lengo la kuhakikisha amani inadumu nchini humo.

Msemaji wa MONUSCO Prosper Félix Basse amesema hayo akijibu swali la wanahabari huko Kinshasa, DRC kuhusu kauli ya afisa mmoja wa Marekani, Tom Pereillo aliyekuwemo ziarani nchini humo hivi karibuni ya kulaani ghasia na kutaka wakiuka haki wafikishwe mbele ya sheria.

Bwana Basse amesema ni lazima wadau wa kisiasa nchini humo wahakikishe kuna mpito wa amani wakati muhula wa rais wa sasa Joseph Kabila unapofikia ukingoni tarehe 19 mwezi huu na kwamba...

(Sauti ya Basse)