Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukimwi huathiri kaya kwa kukosa lishe: FAO

Ukimwi huathiri kaya kwa kukosa lishe: FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO linasema kuongezeka kwa gonjwa la Ukimwi ni tishio kwa maendeleo ya kiuchumi, uhakika wa chakula na lishe hususani katika nchi zenye idadi kubwa ya watu maeneo ya vijijini.

Katika chapisho lake maalum linaloangazia athari za kiafya kwa chakula na lishe, FAO inasema Ukimwi unapoishambulia kaya, wazalishaji ambao ni tegemeo hushindwa kuzalisha, na kwamba hali huwa mbaya zaidi kwani kaya hujikuta ikiuza samani ili kupata chakula na kulipia garama za matibabu hatua inayozidisha umasikini.

Kuafutia hali hiyo shirika hilo linasema linaelimisha umma hususani watunga sera na wataalamu wa maendeleo ili  kujumuisha sera za uhakika wa chakula katika makabiliano dhidi ya Ukimwi.

FAO pia imechukua hatua kadhaa mathalani usaidizi wa uhakika wa chakula na ustawi kwa jamii athirika nchini Msumbiji na Zambia. Katika mpango huo shirika hilo hutoa msaada wa chakula, wafanyakazi na teknolojia.