Machafuko yasababisha vifo 89 Libya :UNSMIL

Machafuko yasababisha vifo 89 Libya :UNSMIL

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL umesema kwa mwezi Novemba umeorodhesha visa 89 vya raia ikiwamo vifo 38 na majeruhi 51 wakati wa matukio ya uhasama nchini humo.

Taarifa ya UNSMIL inasema kuwa kati ya hao watoto wanane waliuawa na wengine 16 walijeruhiwa , huku idadi yanawake watatu wakiuawa na saba kujeruhiwa. Taarifa hiyo pia imetaja wanaume 27 kuawa na watatu kujeruhiwa katika matukio hayo.

Imesema chanzo kikuu cha mauaji hayo ni mashambulizi ya anga, ikuifuatiwa na milio ya risasi, makombora, na mabomu kupitia magari pamoja na vilipuzi.

Kwa mujibu wa ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL, tukio la kusikitisha katika mauaji hayo ni vifo vya kaya moja ambapo baba, na wanawe wakike wawili na wakiume wawili waliuawa mnamo Novemba 26. Miili yao imeonesha alama za risasi na kuchomwa moto.