Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za Fatah zimegeuza wakimbizi kuwa jasiri: Mladenov

Harakati za Fatah zimegeuza wakimbizi kuwa jasiri: Mladenov

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kuhusu amani ya Mashariki ya Kati, Nickolay Mladenov amezungumza huko Ramallah, wakati wa siku ya kuonyesha mshikamano na watu wa Palestina akipongeza kikao cha Saba cha kikukndi cha Fatah kwa kuimarisha mshikamano miongoni mwa wapalestina.

Amewaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa wawe na maazimio ambayo yatahakikisha utambuzi wa mwelekeo wa watu wa Palestina kwa ajili ya kutimiza haki zao za kujitawala, kusaka taifa, heshima na uhuru.

Mwakilishi huo amesema kuwa harakati zao zimegeuza watu waliokuwa wakimbizi kusaka taifa huru na kwamba vizazi vya wapalestina kutoka Gaza na ukingo wa magharibi wa Jordan, Yerusalemu ya Mashariki na kambi za wakimbizi wanasimamia uhuru na kushika nafasi ya kukuza umoja ili kuimarisha mkondo wa siasa Palestina