Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watangaza dola milioni 400 kutokomeza kipindupindu Haiti

UM watangaza dola milioni 400 kutokomeza kipindupindu Haiti

Umoja wa Mataifa leo umetangaza kiasi cha dola milioni 400 kwa kipindi cha miaka miwili ambacho kitatumiwa kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu nchini Haiti.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, ametoa tangazo hilo akisema mkakati huu mpya dhidi ya kipindupindu ulitangazwa mwezi Agosti mwaka jana na utawasilishwa kwa Katibu Mkuu Desemba mosi mwaka huu ambapo unahusiaha maeneo hatua za haraka katika maeneo ambapo matukio yameripotiwa na kusababaisha migogoro ya afya ya umma.

Kwa mujibu wa Dujarric mkakati huo unapendekeza kuanzishwa kwa mpango wa vifaa ya msaada na msaada kwa waliotahirika nchini Haiti.

(SAUTI DUJARRIC)

"Hii ni mbinu ya uwekezaji wa muda mrefu katika vituo vya afya kwakuwa nchi inahitaji kutokomeza kipindupindu; muda mfupi ni uwekezaji wa kuzuia kuenea kwa kipindupindu; na muhimu zaidi, kwamba unaweka watu na jamii athirika na kipindupindu katika moyo wa jitihada zetu, "

Pia ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa

(SAUTI DUJARRIC)

"Hii si suala la kupuuzia kwa ujumla na Katibu Mkuu ana matumaini sana kwamba Baraza Kuu na jumuiya ya kimataifa itaonyesha mshikamano katiakkusaidia Haiti wakati huu nchi anahitaji msaada"