Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukabila, ulemavu na mrengo wa siasa waengue watu kwenye huduma- Ripoti

Ukabila, ulemavu na mrengo wa siasa waengue watu kwenye huduma- Ripoti

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imezinduliwa hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ikisema kuwa katika miongo iliyopita ustawi wa binadamu umepata mafanikio ya aina yake, umaskini ukipungua na afya za watu zikiimarika.

Ikipatiwa jina Ripoti ya hali ya kijamii duniani, umuhimu wa kumjumuisha kila mtu, ripoti hiyo hata hivyo inasema mafanikio hayo hayana uwiano, baadhi ya maeneo yakikumbwa na tofauti za kiuchumi na kijamii miongoni mwa jamii, baadhi ya wananchi wakikumbwa na vikwazo vya kusonga mbele.

Akizungumza na wanahabari mjini New York, Marekani wakati wa uzinduzi, mwandishi kiongozi wa ripoti hiyo Marta Roig amesema ushahidi unaonyesha kuwa kabila, umri, ulemavu na mrengo wa kisiasa ni baadhi ya mambo yanayokwamisha watu kupata ajira, huduma za afya na ujira mdogo.

Ili kupatia suluhu hali hiyo, Bi. Roig amesema hakuna jawabu moja la kisera la kuwezesha ujumuishi bali..

(Sauti ya Martha)

“Ni lazima tuhakikishe kwamba kila mtu yuko tayari kumjumuisha kla mtu na watu wameelimishwa vya kutosha na kuelewa kuwa ujumuishi ni kwa maslahi ya wote, la sivyo tunaweza kuona na tumeshaona upinzani.”