Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

DPRK yawekewa vikwazo kudhibiti upataji wa fedha

DPRK yawekewa vikwazo kudhibiti upataji wa fedha

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo kwa kauli moja limepitisha azimio dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK ambalo pamoja na kulaani jaribio la nyuklia lililofanywa na nchi hiyo tarehe Tisa mwezi Septemba mwaka huu, linaweka vikwazo dhidi ya shughuli zinazopatia fedha serikali ikiwemo kiwango cha biashara ya nje ya makaa ya mawe kwa mwaka.

Azimio hilo liliandaliwa na Marekani ambapo baada ya kupitishwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kila jaribio linalofanywa na DPRK bila shaka linaimarisha teknolojia ya utengenezaji wa silaha hizo ambazo ni hatari kwa binadamu, hivyo amesema..

(Sauti ya Ban)

“Azimio la leo linajumuisha vikwazo vikali na vya kina ambavyo havijawahi kupitishwa na Baraza la Usalama. Linatuma ujumbe mmoja kuwa DPRK lazima isitishe vitendo vyake vya kichochezi na izingatie wajibu wake wa kimataifa.”