Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

DRC ondoeni marufuku ya mikusanyiko kwa wapinzani- Gilmour

DRC ondoeni marufuku ya mikusanyiko kwa wapinzani- Gilmour

Umoja wa Mataifa umeitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuondoa marufuku ya maandamano na mikutano dhidi ya vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia.Taarifa kamili na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Andrew Gilmour amesema hayo leo huko Geneva, Uswisi wakati wa kikao cha kupokea taarifa kuhusu hali ya haki za binadamu kutoka nchi mbali mbali duniani ikiwemo DRC ambako alikuwa ziarani hivi karibuni kwa siku tano.

Amesema upinzani wamepigwa marufuku ilhali chama tawala kinaendelea na maandamano na mikusanyiko kwa madai ya serikali kuwa katazo hilo linalenga kuimarisha usalama kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.

Katika mazungumzo yake na serikali ya DRC..

(Sauti ya Gilmour)

“Niliwaeleza kuwa ni imani yetu kuwa kitendo hiki kitakuwa vinginevyo, kuendelea kukandamiza haki za msingi kutachochea mvutano na bila shaka ghasia zaidi na hivyo usalama kuzorota.”