Skip to main content

Mkakati mpya wa mazingira katika ulinzi wa amani wawasilishwa

Mkakati mpya wa mazingira katika ulinzi wa amani wawasilishwa

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu operesheni za ulinzi wa amani Atul Khare amewasilisha mkakati mpya wa mazingira katika uendeshaji wa operesheni za amani za Umoja wa Mataifa katika Chuo Kikuu cha Columbia hapa mjini New York Jumanne.

Bwana Khare amelezea mtazamo wa idara yake kuwa Ofisi zao kwenye maeneo mbali mbali zinawajibika kufanya kazi katika ufanisi wa kiwango cha juu katika matumizi  ya mali asili, na kutohatarisha watu, jamii na mazingira popote iwezekanavyo.

(Sauti ya Atul)

"Na kulinda mazingira ni lazima tuweke maanani  vitendo tunavyofanya ili kuendeleza mazingira bora. Wajibu wetu ni kuleta amani na pia kuhamasisha matumizi bora ya mazingira yetu kwa njia iliyo sawa. "

Amesema mkakati huo utachukua miaka sita kufikia dhamira hii kwa kuzingatia sera zilizopo, kujifunza kupitia mfumo wa Umoja wa Mataifa, kuhakikisha utendaji ambao ni sambamba na malengo ya maendeleo endelevu katika kulinda  duniani kutokana na uharibifu na usimamizi endelevu wa mali ya asili.

Akiongezea kuwa mkakati huo utaendelea kupewa kipaumbele na kufanyika ukarabati akibainisha changamoto na nguzo tano za msingi  ambazo ni nishati, maji na maji machafu, taka, madhara na mifumo ya usimamizi wa mazingira.

Malengo muhimu ya mkakati huo yanapaswa kufikia mnamo mwaka 20202. Idara yake inasaidia operesheni 36 za  amani  zikiwemo operesheni16 za kulinda amani na  operesheni maalumu 19 za kisiasa katika nchi zaidi ya 30.