Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waliotekeleza ukatili Kivu Kaskazini , DRC kusakwa

Waliotekeleza ukatili Kivu Kaskazini , DRC kusakwa

Serikali ya Jamhuri ya kKidemokrasia ya Congo DRC imesema itahakikisha walitotekeleza unyama na kukatili maisha ya watu 30 wakiwemo wanaume watatu, wanawake 15 na watoto 11 siku ya Jumapili wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Mauaji hayo ylitokea eneo la Luhanga, mji wa Lubero,jimbo la Kivu ya Kaskazini DRC na yanashukiwa kufanywa na wapiganaji wa “Mai-mai Mazembe” walipovamia kambi ya Wahutu waliotawanywa na machafuko, wakiwa wamejihami na bunduki na visu.

Ujumbe wa pamoja wa serikali ya DRC na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO wamezuru eneohilo Jumatatu kutathimini hali halisi na pia kushuhudia wahanga hao wakizikwa.

Dr Martial Kambumbu, ni waziri wa afya wa jimbo hilo

(SAUTI DR KAMBUMBU-KISWAHILI)

Kufuatia mauaji haya ya kikatili wakazi wameanza kufungasha virago na kukimbia maeneo ya jirani.

Habishuti Seninga Robert, ni mbunge wa jimbo la Kivu ya Kaskazini

(SAUTI YA ROBERT)

"Kwanza kabisa suluhu ni kumuelimisha kila mmoja kuanzia washambuliaji, ninamaanisha makundi yenye silaha, kwa sababu wao wenyewe wanaogopa kuuawa. Tunahitaji kuelimisha jamii nzima kuhusu kuishi kwa ajili ya kuishi pamoja kwa amani. Utakubaliana nami kwamba endapo watu hawa wataondoka kwenda Rutshuru, watu wa Rutshuru hawatokubali.Haitakuwa kitu kizuri kama viongozi ni lazima tuzuie na kuwalinda raia popote walipo.”

Duru zinasema sehemu ya kundi la Mai-Mai Mazembe lilishambulia kituo cha jeshio wakati wengine wa kundi hilo wakivamia kambi ya raia.