Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wekeni mazingira bora ya uchaguzi Ghana-Ban

Wekeni mazingira bora ya uchaguzi Ghana-Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Ghana John Dramani Mahama na kiongozi wa chama cha upinzani cha New Patriotic Party (NPP) bwana Nana Addo Dankwa Akufo-Addo.

Ban amezungumza na viongozi hao ikiwa ni siku chache kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika desemba 7 mwaka huu.

Katika taarifa yake iliyotolewa kufuatia mazungumzo hayo Ban amesisitiza umuhimu wa kuweka mazingira mazuri ya kuruhusu uchaguzi huru, wa amani na unaoaminika, akiwataka viongozi hao wawili kuendelea na majukumu yao ya kuhakikisha yanazuia mivutano na kudumisha amani.

Kwa kuzingatia historia ya Ghana ya utulivu wa kisiasa na uchaguzi wa amani, Katibu Mkuu amehimiza haja ya vyama vyote vya kisiasa kutoa saini kanuni za maadili ambazo zitasaidia kupunguza mivutano na kuzuia ghasia za uchaguzi.