Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Uganda na mfalme wa Rwenzururu sakeni suluhu kwa amani- Ban

Serikali ya Uganda na mfalme wa Rwenzururu sakeni suluhu kwa amani- Ban

Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake kufuatia mapigano ya Jumapili kati ya vikosi vya serikali ya Uganda na walinzi wa mfalme Charles Wesley Mumbere wa Rwenzururu yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 50.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric akijibu swali la wanahabari mjini New York, Marekani waliotaka kufahamu kauli ya Umoja wa Mataifa, amesema

(Sauti ya Dujarric)

“Katibu Mkuu ametoa wito kwa pande husika kumaliza tofauti zao kwa amani na kujiepusha na vitendo au kauli zinazoweza kuongeza mvutano.”

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa miongoni mwa waliouawa wakati wa mapigano hayo kwenye jumba la mfalme Mumber huko mji wa Kasese mpakani mwa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ni polisi wa serikali na walinzi wa mfalme.