Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sayansi ina uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko:Ban

Sayansi ina uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko:Ban

Sayansi ina uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko na mchango wake unahitajika zaidi sasa kuliko wakati mwingine wowote . Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Kip-moon akizungumza Jumanne kwenye mkutano kuhusu sayansi na teknolojia kama muwezeshaji wa malengo ya maendeleo endelevu.

Ban amesema ajenda ya mwaka 2030 kwa ajili ya maendeleo endelevu ni mpango wa pamoja kwa ajili ya mustakhbali wa hatua muhimu na kuhakikisha amani na utulivu kwenye sayari dunia.

Ameainisha njia kumi ambazo anatumai jamii ya sayansi inaweza kushiriki katika kutimiza ajenda hiyo ikiwemo Mosi kuitaka jumuiya hiyo kukumbatia malengo ya ajenda ya 2030 na mkataba wa Parisi wa mabadiliko ya tabia nchi.

Pili amesema sayansi inahitajika katika kusaidia kubaini kipi kinawezekana na kipi hakiwezekani, kuanzia masuala ya afya hadi kilimo katika malengo yote na uhusiano uliopo .Tatu Ban ameongeza kuwa dunia inahitaji sayansi kuendelea kutoa ushahidi utakaotoa muongozo wa jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Ban amesisitiza kuwa sayansi itakuwa na sauti kubwa hasa katika kutathimini njia za kutekeleza malengo mengi ikiwemo la kukabili mabadiliko ya tabia nchi.