Viongozi wa Palestina na Israel epukeni kauli chochezi- Thomson

29 Novemba 2016

Leo ni siku ya kimataifa ya kuonyesha mshikamano na watu wa Palestina ambapo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekuwa na mkutano maalum wa kutathmini haki za wapalestina.

Akihutubia hadhira hiyo, Rais wa Baraza Kuu Peter Thomson, amepongeza kamati ya baraza hilo inayohusika na ufuatiliaji wa haki za wapalestina, akigusia mafanikio yaliyopatikana ikiwemo Palestina kupata hadhi ya uangalizi kwenye Umoja wa Mataifa na bendera yake kupeperushwa kuanzia mwaka jana.

Hata hivyo amesema bado kuna changamoto ikiwemo vikwazo huko Gaza na mazingira mengine yanayosababisha kuyoyote kwa suluhu ya uwepo wa mataifa mawili, hivyo amesema..

(Sauti ya Thomson)

“Nasihi viongozi wa Israeli na Palestina kuondoa mvutano na kujizuia kufanya ghasia na utoaji wa kauli chochezi zinazosababishwa amani ishindwe kufikiwa.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter