Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM inagawa msaada wa dharura kwa familia zilizothirika na vita Somalia

IOM inagawa msaada wa dharura kwa familia zilizothirika na vita Somalia

Shirika la Umoja wa Mataifa ya Uhamiaji  IOM nchini Somalia linagawa msaada wa dharura vikiwemo vyandarua vya mbu, maturubai, mablanketi, magodoro, mazulia na vifaa vya usafi kwa familia 100 zilizotawanywa na mapigano mjini Galkaayo, Somalia, kwa ufadhili wa serikali ya Japan.

Kwa mujibu wa Dr. Chaiki Ito mkuu wa IOM Somalia wamefanya tathimini kwa ushirikiano na mashirika mengine ya kibinadamu ili kubaini mahitaji ya muhimu nay a haraka kwa familia hizo zilizokimbia vita.

Miongoni mwa waliopokea msaada huo wamesema wamekimbia bila kitu chochote kuokoa maisha yao baada ya wengine kushuhudia nyumba zao zimechomwa moto, hivyo wamesema msaada huu utawasaidia sana.