Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujipima mwenye VVU kutapanua wigo wa huduma- WHO

Kujipima mwenye VVU kutapanua wigo wa huduma- WHO

Kuelekea siku ya Ukimwi duniani tarehe mosi mwezi ujao, shirika la afya duniani, WHO limetangaza mwongozo mpya wa kujipima Virusi Vya Ukimwi, VVU kwa lengo la kupanua upatikanaji wa huduma hiyo na uchunguzi wa virusi hivyo. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Mwongozo huo unahusisha mtu kuchukua vitendanishi na kujipima kwa kutumia majimaji ya mwilini au damu kutoka kidoleni na kubaini iwapo ana virusi au la na majibu anapata ndani ya dakika 20 au chini ya hapo.

WHO inasema iwapo majibu yanakuwa chanya, mtu huyo analazimika kwenda kituo cha afya na kusaka uhakika wa matokeo hayo ambapo ikiwa yatathibishwa, atapatiwa ushauri nasaha na huduma nyingine za matibabu ikiwemo dawa.

Rachel Baggaley, mratibu katika idara ya Ukimwi WHO anafafanua kwa wale ambao watajipima na kubaini hawana VVU.

(Sauti ya Baggley)

“Iwapo umekuwa na mahusiano karibuni, kwa sababu kuna muda maalum wa hadi wiki sita ambapo vikinga mwili vinajitengeneza, vitendanishi hivi havitaweza kubaini maambukizi ya virusi, hivyo wanashauriwa kujipima tena baada ya wiki sita.”

WHO inasema mwongozo mpya ni muhimu kwa kutafungua milango zaidi kufikia watu wengi na ni njia mojawapo ya kuwapatia watu uwezo juu ya afya zao na kusogeza huduma karibu na wananchi.